Siku ya Umoja wa Mataifa yaadhimishwa nchini Ethiopia
2024-10-25 09:26:58| CRI

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na jumuiya za kidiplomasia nchini Ethiopia zimesherehekea Siku ya Umoja wa Mataifa jana Alhamis katika makao makuu ya Kamisheni ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) mjini Addis Ababa, huku zikitoa wito wa kuanzisha mfumo wa usimamizi wa dunia wenye usawa zaidi na mwitikio wa haraka zaidi.

Siku ya Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kukumbuka siku ya kuanza kufanya kazi kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa mwaka 1945, inayolenga kuhimiza amani, usalama, maendeleo na haki za binadamu kote duniani.

Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia Bw. Ramiz Alakbarov amesisitiza haja ya kupunguza mvutano, kutokomeza umaskini na kukuza maendeleo endelevu duniani kote.