Zambia jana iliadhimisha miaka 60 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza, ambapo rais Hakainde Hichilema amelitaka taifa hilo lirejeshe ahadi yake ya kujenga mustakabali mwema.
Katika hotuba yake iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa, rais Hichilema ameonyesha matumaini kwa mustakabali wa nchi hiyo, akisisitiza kuwa Zambia itaendelea kung'aa na kuwa na mshikamano katika amani na malengo katika miaka 60 ijayo na zaidi kwa kupitia juhudi za pamoja.
Rais Hichilema amesema Zambia lazima ikabiliane na changamoto za kisasa kama vile mabadiliko ya tabia nchi na rushwa kwa uzalendo na imani, na kujitahidi kujenga taifa lenye haki na ustawi.