Rais wa China Xi Jinping ametaka juhudi zaidi zifanyike ili kutimiza mafanikio katika sekta ya sayansi na teknolojia ya baharini.
Rais Xi amesema hayo alipojibu barua kwa walimu na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha masuala ya Baharini cha China kilipotimia miaka 100 ya kuasisiwa kwake. Kwenye barua yake, rais Xi amekitaka Chuo Kikuu hicho kuchukulia miaka hiyo 100 kama mwanzo mpya, kuongeza juhudi zaidi ili kutimiza mafanikio ya kisayansi na kiteknolojia ya ubunifu, na kulea vipaji bora zaidi ili kuchangia katika kujenga China kuwa nchi inayoongoza katika elimu na nchi yenye nguvu za baharini.