Botswana yakabidhiwa shule ya nne inayosaidiwa na China
2024-10-28 09:36:03| CRI

Botswana Jumapili ilikabidhiwa rasmi shule ya msingi ya nne inayosaidiwa na China.

Shule ya Msingi ya Ramaeba iliyopo kijiji cha Kazungula, kaskazini mwa Botswana, ina ukubwa wa takriban mita za mraba elfu 61 ambapo ndani yake kuna madarasa 14 yanayoweza kubeba wanafunzi 560, pia ina majengo 16, ikiwa ni pamoja na jengo la kufundishia, ofisi, maktaba, mgahawa, bweni la walimu na uwanja wa michezo.

Balozi wa China nchini Botswana Bw. Fan Yong amesema China imetambua kuwa elimu ni kitu muhimu zaidi kwenye mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Botswana.

Hafla hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa na rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana, makamu wa rais Slumber Tsogwane na maofisa wengine wa ngazi ya juu. Tsogwane amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni ushahidi wa ushirikiano imara kati ya Botswana na China.