Botswana imezindua rasmi ubunifu wake mpya wa usafiri wa vyombo vya umeme, yaani Boti ya Umeme (eBoat), ikiashiria hatua muhimu katika azma yake ya kufikia usafiri wa vyombo vya umeme.
Mpango huu ni nyongeza katika bidhaa mfululizo za usafiri wa kijani uliozinduliwa na serikali katika wiki za karibuni, kama ilivyosisitizwa na Rais Mokgweetsi Masisi katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Makamu wa Rais Slumber Tsogwane siku ya Jumapili katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika kitongoji cha mapumziko cha Kasane kilichopo kaskazini-magharibi mwa Botswana.
Tsogwane amesema Botswana inaendana na malengo yaliyoainishwa katika Mkakati wake wa Mpito wa Nishati, unaolenga kuongeza matumizi ya vyanzo vya nishati safi katika sekta mbalimbali, ikiwemo uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma.
Mapema mwezi huu, Botswana ilizindua magari yake ya kwanza ya umeme yaliyounganishwa mjini Gaborone, kwa msaada wa makampuni mawili ya utengenezaji wa magari ya China.