Idadi ya vifo vya wapalestina yazidi 43,000 huko Gaza
2024-10-29 09:59:13| CRI

Idadi ya vifo vya wapalestina vilivyotokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imezidi 43,000 hadi kufikia Jumatatu, wakati vikosi vya Israel vikiendelea kushambulia maeneo mbalimbali nchini Lebanon na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 2,710 tangu mapigano kati ya Israel na kundi la Hezbollah yazuke Oktoba mwaka jana.

Mamlaka za afya huko Gaza zimetoa taarifa ikisema, katika saa 48 zilizopita, jeshi la Israel limewaua watu 96 na kuwajeruhi wengine 277 huko Gaza, na kufanya idadi ya vifo kufikia 43,020 na idadi ya majeruhi kufikia 101,110 tangu kuzuka kwa mapigano kati ya Palestina na Israel Oktoba 7 mwaka 2023.

Jeshi la IDF la Israel limetoa taarifa ikisema, vikosi hivyo vilifanya mashambulizi ya kulenga katika maeneo ya katikati na kusini mwa Gaza, yakiwaua wapiganaji wenye silaha na kubomoa miundombinu yao.