Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi ameziagiza taasisi zinazosimamia masoko mapya kuweka viwango vidogo vya malipo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili wamudu kulipa na kuendelea na biashara katika mazingira mazuri.
Rais Mwinyi amesema hayo alipofungua soko jipya la kisasa la Jumbi, Mkoa wa Mjini Magharibi, na kuwahakikishia wafanyabiashara kuwa serikali itaendelea kuwaandalia mazingira bora zaidi yatakayoendana na soko hilo.
Rais Mwinyi amesisitiza kuwa serikali imetenga shillingi bilioni 100 kwa ajili ya kuwapatia mitaji wajasiriamali na wafanyabiashara kuimarisha biashara zao.