Watu 7 wafariki baada ya jengo kuporomoka katika mji mkuu wa Nigeria
2024-10-29 10:03:44| CRI

Takriban miili saba imepatikana kutoka kwenye vifusi baada ya jengo lililobomolewa nusu kuporomoka siku ya Jumamosi katika eneo la kitongoji cha Sabon-Lugbe cha Abuja nchini Nigeria.

Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Majanga ya Eneo la Mji Mkuu Abdulrahman Mohammed amesema kwamba jengo hilo liliporomoka baada ya kundi la watu wanaoshukiwa kuwa waharibifu kuingia ndani wakivuta na kubeba nondo kwenye jengo hilo.

Mohammed ameongeza kuwa kitendo hiki cha washukiwa kimesababisha sehemu iliyobaki ya jengo lililobomolewa kuwaangukia, na majeruhi wawili waliokolewa na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.