UNECA yasema takwimu sahihi na za wakati ni muhimu katika kukabiliana na majanga yanayoongezeka
2024-10-29 10:37:55| cri

Mkurugenzi wa Kituo cha Takwimu cha Afrika kilicho chini ya Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Oliver Chinganya amesema, takwimu za ubora wa juu zinazohusiana na majanga zinahitajika sana wakati bara la Afrika na dunia kwa ujumla linakabiliwa na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi na majanga mengine.

Chinyanga amesema hayo wakati akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa 4 wa Wataalamu wa Kimataifa wa Watengenezaji na Watumiaji wa Takwimu zinazohusiana na Majanga unaofanyika Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, kuanzia Oktoba 28 hadi Novemba Mosi.

Amesisitiza kuwa, katika mazingira ya sasa ambapo majanga yanayotokana na vitendo vya binadamu na ya asili yanayongezeka barani Afrika na sehemu nyingine duniani, takwimu husika zinazohusiana na majanga ni muhimu ili kuweza kujibu kwa usahihi na kushughulikia majanga yaliyopo sasa na yanayoweza kutokea katika siku za baadaye.