Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi amesisitiza haja ya juhudi za pamoja za kimataifa katika kutimiza kusimamisha vita mara moja katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu mjini Cairo imesema, Rais Sisi amesema hayo alipokutana na mwenyekiti wa Chama cha Watu wa Ulaya, Manfred Weber. Rais Sisi pia amesisitiza kuwa suluhisho la nchi mbili na kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina kwa kuendana na maazimio halali ya kimataifa, ni njia pekee ya kutimiza amani ya kudumu na utulivu katika kanda hiyo.
Kwa upande wake, Weber amepongeza nafasi ya Misri katika kuboresha utulivu wa kikanda na juhudi zake katika kushughulikia migogoro kwenye kanda hiyo.