Ni dalili gani za Ukomo wa Hedhi na Je wanawake wote wanapata dalili hizi
2024-11-01 08:32:06| CRI

Kukoma hedhi ni sehemu ya asili ya kuzeeka kwa wanawake, kwani kipindi hiki ovari huacha kufanya kazi kwa sababu ya kupungua kwa homoni za uzazi. Utambuzi wa kukoma hedhi hufanywa baada ya mwanamke kukosa hedhi kwa miezi 12 mfululizo. Huu ni mchakato wa taratibu sana, kuanzia sababu, ambapo hedhi inakuwa isiyo ya kawaida kabla ya kuacha kabisa. Hivyo katika kuenzi hali hii ya wanawake na kuwashika mkono kwa kuwaonesha kuwa watu wako pamoja nao, kila ifikapo tarehe 18 Oktoba ya kila mwaka dunia inaadhimisha Siku ya Ukomo wa Hedhi, ikiwa na lengo la kuongeza uelewa na kuondoa unyanyapaa wanaokumbana nao mamilioni ya wanawake wanaopitia hali hiyo ya kibiolojia.

Kwa sasa idadi ya wanawake waliofikia ukomo wa hedhi inaongezeka kwani kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa wanawake wanaishi muda mrefu zaidi ikilinganishwa na wanaume. Mwaka 2021, wanawake wenye umri wa miaka 50 na zaidi walikuwa 26% ya wanawake na wasichana wote duniani idadi ambayo imeongezeka kutoka 22% ya miaka 10 nyuma. Kawaida umri wa kukoma hedhi huanza miaka 45 mapaka 55 huku wastani ukiwa ni miaka 51, hata hivyo pia inatagemea na mwanamke mwenyewe, kuna wengine wanakoma hedhi hata wakiwa na umri wa miaka chini ya 40. Licha ya ukomo wa hedhi kuwa hatua ya kawaida katika maisha ya mwanamke mara nyingi huwa haieleweki. Hivyo leo kwenye kipindi cha ukumbi wa wanawake tutaangalia dalili gani za Ukomo wa Hedhi na Je wanawake wote wanapata dalili hizi.