Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Finland Alexander Stubb hapa Beijing.
Rais Xi amesema, Finland ni moja kati ya nchi za kwanza za magharibi zilizoanzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China na nchi ya kwanza ya magahribi kusaini makubaliano ya biashara kati ya serikali na China.
Pia amesema, tangu China na Finland zianzishe uhusiano wa kibalozi, siku zote pande mbili zinadumisha uhusiano wa kirafiki kwenye msingi wa kuheshimiana na kuaminiana, huku zikiweka mfano wa kuigwa wa uhusiano wa nchi na nchi unaovuka tofauti za historia, utamaduni na mifumo, na kuhimiza mawasiliano yenye usawa.
Rais Xi ameongeza kuwa China inapenda kufanya juhudi pamoja na Finland kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, kuendeleza urafiki wa jadi na kuzidi kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano ili kunufaisha zaidi nchi mbili na watu wao na kutoa mchango mpya kwa amani na maendeleo ya dunia.