Idara ya Anga ya juu ya China (CMSA) imetangaza kuwa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-19 ikimerushwa kwa mafanikio.
Chombo hicho kimetuma wanaanga watatu, akiwemo mhandisi wa anga wa kwanza wa kike nchini kwenye kituo chake cha anga ya juu kwa misheni ya miezi sita.
Chombo hicho kilicho juu ya roketi ya kubebea ya Long March-2F, kilirushwa saa 10:27 alfajiri kutoka Kituo cha Kurushia Satelaiti cha Jiuquan kaskazini magharibi mwa China. Takriban dakika 10 baada ya kurushwa, chombo cha Shenzhou-19 kilijitenga na roketi na kuingia kwenye obiti yake iliyoteuliwa.
Shenzhou-19 ni safari ya misheni ya 33 katika mpango wa China wa kutuma binadamu kwenye anga ya juu na ni safari ya misheni ya nne ya kutuma wanaanga wakati wa hatua ya matumizi na maendeleo ya kituo cha anga cha China.