Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Dk Damas Ndumbaro amekagua miundombinu ya michezo katika uwanja wa Shule Kuu ya Sheria na Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam ambavyo vitatumika kwa mazoezi wakati wa fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN 2025) na Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2027).
Katika ziara hiyo ya ukaguzi, Dk. Ndumbaro, akiwa ameambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, amesema hadi sasa hatua iliyofikiwa inakidhi vigezo kuelekea katika mashindano hayo.
Kwa mara ya kwanza Tanzania, Kenya na Uganda zitakuwa wenyeji wa mashindano hayo.