Namibia yakabidhiwa shule nne zinazosaidiwa na China
2024-10-30 09:43:27| CRI

Serikali ya Namibia Jumatatu ilikabidhiwa shule nne zinazosaidiwa na China zilizoko katika mikoa ya Kavango Magharibi na Zambezi nchini Namibia.

Ujenzi wa shule hizo nne zikiwemo Shule ya Msingi ya Satotwa na Shule ya Muungano ya Simanya zilizoko Kavango Magharibi, Shule ya Muungano ya Liselo na Shule ya Muungano ya Masokotwani zilizoko Zambezi ulianza mwezi Machi mwaka 2022 chini ya uungaji mkono wa serikali ya China. Shule hizo zina hosteli, nyumba za walimu, majengo ya utawala, madarasa, sehemu za kunawa, maktaba na vitanda, ambapo wanafunzi takriban 1,200 watanufaika.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa wa Namibia Lukas Sinimbo Muha alisema shule hizo zitasaidia kupunguza kiwango cha wanafunzi wanaoacha shule na kupunguza walimu kuacha kazi.

Balozi wa China nchini Namibia Bw. Zhao Weiping alisema shule zinazojengwa kwa msaada wa China ni alama mpya ya urafiki kati ya China na Namibia. China siku zote inaunga mkono maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Namibia, na kutoa kipaumbele kwa elimu katika ushirikiano wake na Namibia.