China na Zambia zaadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia
2024-10-30 09:47:06| CRI

China na Zambia Jumanne zilifanya sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Sherehe hiyo ilifanyika katika Hifadhi ya Kumbukumbu ya TAZARA katika Wilaya ya Chongwe, mashariki mwa Lusaka, Zambia. Shughuli ya kuweka mashada ya maua ilifanyika kwa heshima ya raia wa China waliofariki dunia wakati wa ujenzi wa njia ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Maadhimisho hayo yaliyofanyika chini ya kaulimbiu "Kurithisha moyo wa TAZARA kwa kizazi kijacho na kujenga kwa pamoja mustakabali wa pamoja", ilihudhuriwa na Balozi wa China nchini Zambia Han Jing na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema pamoja na maofisa wa Ubalozi wa China na Serikali ya Zambia.

Katika hotuba yake, balozi wa China alitoa shukrani kwa viongozi waanzilishi wa nchi hizo mbili kwa kuanzisha uhusiano wa muda mrefu ambao umesimama kwa muda mrefu na umeonekana kuwa mfano mzuri wa uhusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa Kusini na Kusini.