Shirika la Uhamiaji la Kimataifa IOM limesema, zaidi ya watu milioni 14 wamekimbia makaazi yao tangu kuzuka wa mapigano yanayoendelea nchini Sudan.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la IOM Bi Amy Pope ametoa taarifa akisema, idadi ya wakimbizi wa ndani imefikia milioni 11, huku idadi hiyo ikiongezeka kwa laki 2 tangu mwezi wa Septemba.
Ameongeza kuwa wengine milioni 3.1 wamevuka mipaka kukimbia mapigano hayo. Kwa ujumla asilimia 30 ya watu wote wa Sudan wamepoteza makazi.
Bi Pope ameeleza hali nchini Sudan kama maafa, huku akisema mateso yanaongezeka siku hadi siku na watu takriban milioni 25 wanahitaji misaada.