WTO laendesha kongamano juu ya matokeo ya biashara na uchumi ya mkutano wa FOCAC wa Beijing
2024-10-31 09:57:34| CRI

Shirika la Biashara Duniani (WTO) tarehe 30 liliendesha kongamano lenye kauli mbiu ya “Mtazamo wa WTO juu ya ushirikiano kati ya China na Afrika” mjini Geneva nchini Uswisi, ambapo linafuatilia matokeo ya biashara na uchumi ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Kongamano hilo lilijadili matokeo muhimu yanayopatikana kwenye mkutano wa FOCAC wa Beijing, kuelezea mifano ya China ya kutoa msaada kwa nchi zilizo nyuma zaidi kiuchumi, na kajadili uwezekano wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuhimiza mageuzi ya WTO na kuendeleza kwa pamoja uhusiano wa kiwenzi na kiuchumi.

Washiriki wa kongamano hilo wanaona kuwa hatua ya kiwenzi ya kustawisha biashara kati ya China na Afrika itaendelea kuwa chachu kwenye ushirikiano wa pande hizo mbili.