Serikali ya Tanzania imeikumbusha jumuiya ya kimataifa hususan nchi zilizoendelea kutekeleza jukumu lake na kuwezesha upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa Mkakati wa Dunia wa kuhifadhi Bioanuai kuendana na ibara ya 20 na 21 ya Mkataba wa Bioanuai.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk Ashatu Kijaji amesema hayo alipomwakilisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi wa Uhifadhi wa Mazingira unaofanyika jijini Cali, Colombia.
Sanjari na hilo, Dk Kijaji amewakumbusha wadau kutoka nchi zinazoendelea kuwekeza rasilimali zitakazowezesha utekelezaji wa mikakati hiyo kuwezesha fedha za kuhifadhi bionauai katika nchi zinazoendelea.