Mkutano wa Kilele wa Teknolojia ya Afya barani Afrika umeanza jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, kwa kutoa wito kwa wataalamu wa afya na wavumbuzi kutumia teknolojia za afya ili kujenga unyumbufu na kuboresha mifumo ya afya barani Afrika.
Mkutano wa tatu wa Teknolojia ya Afya barani Afrika ulioanza jumanne na unamalizika hii leo, umekutanisha mawaziri wa afya na wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), wavumbuzi wa teknolojia na wataalamu wa afya kutoka barani Afrika.
Chini ya kaulimbiu ya “Uvumbuzi kwa ajili ya Afya ya Jamii: Kufungua Nguvu ya Akili Bandia,” wajumbe watatafiti njia za kutimiza fursa ya uvumbuzi ikiwemo akili bandia, mtandao wa vitu, roboti na droni ili kukabiliana na changamoto kubwa za kiafya barani Afrika.
Washiriki wamesema kuimarisha uhusiano katika sekta zote ni ufunguo wa kujenga mifumo bora ya afya iliyo tayari kukabiliana na majanga yoyote kwa wakati.