Watu wanane wafariki dunia katika ajali ya kuporomoka kwa mgodi nchini Zambia
2024-10-31 09:59:12| CRI

Polisi wa Zambia wamesema watu wanane wamefariki dunia, sita kati yao wakiwa wa familia moja, na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya mgodi wa shaba kuporomoka katika eneo la Chingola katika Mkoa wa Copperbelt katikati mwa nchi hiyo.

Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Copperbelt, Mwemba amesema kuwa wachimbaji haramu kadhaa walikuwa wakichimba madini ya shaba wakati tukio hilo likitokea, na baadhi yao walizikwa na vifusi.

Hivi sasa Zambia ipo kwenye msimu wa mvua, na udongo wa unyevu unaongeza hatari ya kuporomoka kwa mgodi. Habari zimesema kuwa uchimbaji haramu wa madini ni jambo la kawaida katika maeneo ya uchimbaji madini ya Zambia. Kutokana na kukosekana kwa hatua muhimu za ulinzi, ajali zinatokea mara kwa mara.