IOM yasema zaidi ya watu milioni 14 nchini Sudan wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano
2024-10-31 22:55:08| cri

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema kuwa zaidi ya watu milioni 14 wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa mapigano yanayoendelea nchini Sudan.

Mkurugenzi Mtendaji wa IOM Amy Pope amesema, idadi ya wakimbizi wa ndani imefikia milioni 11, na watu wengine milioni 3.1 wamekimbilia nchi jirani kukwepa mapigano hayo.

Pope ameelezea hali ya nchini Sudan kuwa ni janga, na kuongeza kuwa karibu watu milioni 25 nchini humo wanahitaji msaada kwa sasa.

Sudan imeshuhudia mapigano makali kati ya Jeshi la nchi hiyo na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) yaliyoanza April 15 mwaka jana.