Waziri wa Afya nchini Sudan, Haitham Mohamed Ibrahim amesema, kiwango cha vifo vya wamama wajawazito nchini humo kimeongezeka na kufikia 295 kati ya 200,000, na kile cha watoto wachanga kimeongezeka kwa 51 kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa.
Katika taarifa yake, Bi. Haitham amesema, afya ya mama na watoto inahitaji huduma maalum baada ya kuongezeka kwa vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga kutokana na vita inayoendelea nchini humo.
Waziri huyo ameeleza mpango mkakati wa mwaka 2025 unaolenga kuboresha afya ya wamama na watoto utakagharimu dola za kimarekani milioni 200, na kusisitiza haja ya kuunganisha juhudi za wizara ya afya na wenzi wa kimataifa ili kupunguza kiwango cha vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga.