Donald Trump akadiriwa kushinda urais baada ya kupata kura 270 kati ya 538
2024-11-06 15:39:12| cri

Vyombo vya habari vya Marekani vimekadiria kuwa mgombea wa Chama cha Republican Donald Trump atapata ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo baada ya kunyakua kura 270 kati ya zote 538, na chama chake pia kitachukua udhibiti wa Baraza la Seneti kufuatia kunyakua viti 51 kati ya 100.