Utalii na utamaduni vinasaidia kuweka msingi wa uhusiano kati ya China na Tanzania
2024-11-06 08:51:43| CRI

Maofisa wa ngazi ya juu kutoka serikali za China na Tanzania wametangaza utalii na utamaduni  kuwa ni mambo mawili yanayosaidia kuimarisha msingi wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Hayo yamesema katika hafla ya kufungwa kwa sherehe za Mwaka wa Utalii na Utamaduni kati ya Tanzania na China kwa mwaka 2024 na pia kusherehekea miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili zilizofanyika jijini Dar es Salaam jumatatu usiku.

Wakizungumza katika hafla hiyo, maofisa hao wamesema utalii na utamaduni sio tu vinasaidia kuchochea maendeleo ya uchumi, lakini pia zinasaidia kuboresha mawasiliano kati ya watu na watu na kuongeza maelewano kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Pindi Chana amesema, uhusiano kati ya Tanzania na China umeendelea kukua, na kupata matokeo mazuri katika ushirikiano wa kivitendo na  mawasiliano ya kitamaduni.

Naye Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema, China na Tanzania  kila upande una utamaduni wake wa historia ndefu, na kuwa na maisha ya masikilizano katika mazingira ya amani.