Waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang jana huko Shanghai ameshiriki na kuhutubia ufunguzi wa Maonesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE).
Kwenye hotuba yake, Bw. Li amesema, kufanya maonesho hayo ni hatua muhimu ya China katika kupanua ushirikiano na ufunguaji mlango, na pia ni ahadi muhimu iliyotolewa na China kwa dunia.
Bw. Li ametoa mapendekezo matatu, ambayo ni kuzitaka pande mbalimbali zifikie maoni ya pamoja kuhusu kufungua mlango na kufanya ushirikiano kwa msingi wa kuimarisha uaminifu na kushikilia ahadi zao, amezitaka pande mbalimbali kupanua ushirikiano zaidi kwa msingi wa kunufaishana na kupata maendeleo, na pia amezitaka pande mbalimbali zibebe majukumu ya kufungua mlango kwa msingi wa kushikilia jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja.