Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yameendelea kuvunja rekodi mbalimbali, kwani kampuni 3,496 kutoka nchi na sehemu 129 zinashiriki, zikiwemo kampuni 297 zilizoko kwenye orodha ya kampuni 500 tajiri zaidi duniani, na kampuni na taasisi 186 kati ya hizo zimeshiriki kwenye awamu zote saba za maonyesho ya CIIE.
Matokeo ya kura za maoni zilizofanywa na CGTN yameonyesha kuwa, asilimia 67 ya wahojiwa wanaona China ni soko huru lenye uwazi na ushindani.
Uwazi ni dhana kuu ya Maonyesho ya CIIE, pia ni alama dhahiri ya njia ya China kuelekea kuwa nchi ya kisasa. Takwimu zinaonyesha kuwa, katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, thamani ya jumla ya uuzaji wa bidhaa za China kwa nje na uagizaji bidhaa kutoka nje imefikia kiwango cha juu zaidi.
Matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa, asilimia 77.5 ya waliohojiwa wanaona mazingira ya kibiashara ya China yanavutia wawekezaji, asilimia 73.9 wanaunga mkono nchi zao na kampuni za nchi zao kushiriki kwenye miradi ya ushirikiano ya kimataifa iliyoanzishwa na China, asilimia 78.5 wanaona nchi zao na kampuni za nchi zao zinapata faida kutokana na biashara na China, na wanaamini ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa China utatoa fursa nyingi zaidi kwa washirika wake wa kibiashara.
Aidha, asilimia 84.3 ya wahojiwa wanaona China ni muhimu kwa ajili ya utulivu wa minyororo ya uzalishaji na ugavi duniani.
Maonyesho ya CIIE ya mwaka huu yameweka maeneo ya mabanda zaidi 120 ya bila malipo kwa nchi 37 zilizoko nyuma kimaendeleo, na kupunua eneo maalumu la bidhaa za Afrika, ili kufungua mlango zaidi kwa nchi hizo.
Asilimia 89.9 ya watu kutoka Afrika waliohojiwa wanapongeza hatua ya China ya kufuatilia na kuunga mkono nchi za Kusini, asilimia 78.2 wanaona China inashikilia kuunganisha maendeleo yake yenyewe na maendeleo ya Afrika, kuunganisha kwa karibu fursa ya maendeleo ya China na fursa ya maendeleo ya Afrika, asilimia 92.1 wanaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye miradi ya ushirikiano wa kimataifa inayoanzishwa na China.
Jumuiya ya kimataifa ina imani kubwa juu ya mustakabali wa uchumi wa China na soko la China.
Matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa, asilimia 92.3 ya wahojiwa wamepongeza maendeleo imara ya uchumi wa China, asilimia 91.9 wanaona uchumi wa China unakua kwa kasi, asilimia 81.3 wanaona mwelekeo wa kimsingi wa ukuaji wa uchumi wa China haujabadilika, na asilimia 89.2 wamesifu mchango mkubwa wa China kwa uchumi wa dunia katika miaka ya hivi karibuni.