Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Salim Mvurya Jumanne alisema, Kenya itapanua sekta ya uzalishaji viwandani isiyosababisha uchafuzi kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa nishati endelevu na teknolojia mpya, ili kuhimiza uuzaji wa bidhaa nje na kutoa nafasi mpya za ajira.
Bw. Mvurya amesema serikali imeweka sera na sheria kwa ajili ya kuhimiza sekta hiyo ibadilike kuwa sekta isiyotoa hewa ya ukaa, ambayo inatarajiwa kutimiza marekebisho ya tabianchi na ukuaji shirikishi wa uchumi.
Ameongeza kuwa Kenya inahimiza maendeleo ya sekta ya uzalishaji viwandani isiyosababisha uchafuzi, hali ambayo inaipa sekta hiyo nafasi ya matumizi ya teklonojia mpya ikiwa ni pamoja na akili bandia.