Raia 10 wauawa katika shambulio lililofanywa na kikosi cha RSF katikati ya Sudan
2024-11-06 08:50:42| CRI

Raia 10 wameuawa katika shambulio lililofanywa na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) katika kijiji cha Al-Barorab, mkoa za Gezira katikati ya Sudan.

Wakati huohuo, Mtandao wa Madaktari nchini Sudan umethibitisha kuwa, watu 13 wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na wapiganaji wa kikosi cha RSF katika kijiji cha Al-Barorab jumatatu jioni. Mtandao huo umelaani mauaji na uporaji katika vijiji vya mkoa wa Gezira, na pia hatua ya kuzingira eneo hilo ambayo imesababisha watu wengi kukimbia makazi yao na janga kubwa la kibinadamu.

Katika ripoti yake iliyotolewa jana jumanne, Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, karibu watu 135,400 wamekimbia makazi yao kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Gaza kufuatia kuongezeka kwa mapigano katika zaidi ya vijiji na miji 30 mkoani humo tangu Oktoba 20 mwaka huu.