Muungano wa utawala wa taifa wa Iraq wapinga kauli ya kuanzisha mashambulizi kwa kutumia ardhi ya Iraq
2024-11-07 10:51:00| cri

Muungano wa utawala wa taifa wa Iraq tarehe 6 Novemba ulikutana kujadili masuala makuu na hali ya maendeleo ya sasa huko Iraq, na kufanya mazungumzo juu ya marekebisho ya baraza la mawaziri yatakayofanyika nchini humo.

Mkutano huo ulisisitiza msimamo wa Iraq kwa kuunga mkono watu wa Palestina na Lebanon katika kupinga mashambulizi ya Israel, na kulaani “makosa ya mauaji ya kimbari” ya Israel dhidi ya raia.

Mkutano huo pia ulipinga kauli ya kutumia ardhi ya Iraq kama mahali pa kuanzisha mashambulizi, ukisema kauli husika “haina msingi wowote”, ila ni kisingizio cha kukiuka mamlaka na ardhi ya Iraq. Mkutano huo ulisisitiza kufanya juhudi kwa pamoja, kuweka kipaumbele maslahi makuu ya Iraq, kuepuka vita nchini Iraq, kuzuia Israel katika kupanua mapambano na kuzuia Iraq itumbukie kwenye ukosefu wa usalama.