Hivi karibuni hapa China walisherehekea siku maarufu sana ya manunuzi yaani Novemba 11 ama 11/11. Ingawa siku hii asili yake ni siku ya mabechela yaani watu wote wasioukuwa kwenye uhusiano, lakini baadaye iligeuka na kuwa siku ya manunuzi baada ya wafanyabiashara kuona njia nzuri ya kuwaliwaza mabachela hawa ni kuwapunguzia bei bidhaa. Tarehe, 11 Novemba (11/11), ilichaguliwa kwa sababu nambari 1 inafanana na mkwaju mtupu kwa maandishi ya Kichina, nah ii ni lugha kimtandao kwa Wachina kwa mwanamume ambaye hajaoa na kushindwa 'matawi' yaani ukoo kwenye familia. Cha kushangaza, sikukuu hiyo ikakuwa maarufu ya kusherehekea uhusiano ambapo zaidi ya wanandoa 4,000 walifunga ndoa hapa Beijing mwaka 2011, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko wastani wa kila siku wa ndoa 700.
Hata hivyo, mwaka 2009 Mkurugenzi Mtendaji wa Alibaba Daniel Zhang alianza kutumia siku hiyo kama tamasha la siku ya manunuzi kwa saa 24 na kutoa punguzo la manunuzi mtandaoni pamoja na burudani ya nje ya mtandao. Siku hii sasa imekuwa kubwa zaidi ya manunuzi ya rejareja na mtandaoni duniani. Washindani wa Alibaba, kama vile JD.com nao huandaa tamasha la mabechela pia, ambalo liliingiza dola za Marekani bilioni 19.1, na kufikisha jumla ya mauzo ya China hadi dola bilioni 44.5 mwaka wa 2017. Wanunuzi wa Alibaba walizidi Yuan bilioni 213.5 (dola za Marekani bilioni 30.7) kwenye matumizi yao ya jumla katika Siku ya Watu Wasio na Wapenzi yam waka 2018. Na kwa kuwa tunafahamu kuwa manunuzi huwa yanafanywa zaidi na wanawake, hivyo leo katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake tutaangalia Wanawake na manunuzi katika siku ya 11/11.