Xi atuma salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka mia moja ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Sun Yat-sen
2024-11-12 23:06:11| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya miaka mia moja ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Sun Yat-sen siku ya Jumanne.

Xi amehimiza chuo kikuu hicho kuoanisha maendeleo yake na mikakati mikuu ya kitaifa na mahitaji ya maendeleo ya eneo la ghuba kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao.