Mwamuzi wa Premier League Coote asimamishwa kazi baada ya video kumuonyesha akimtusi Klopp wa Liverpool
2024-11-12 14:47:47| cri

Mwamuzi wa Premier League David Coote amesimamishwa na bodi ya waamuzi PGMOL siku ya Jumatatu ili kupisha uchunguzi kamili baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha afisa huyo akidaiwa kuitusi Liverpool na meneja wake wa zamani Juergen Klopp.

Video inayodaiwa inamuonyesha Coote akitoa kauli za dharau kuhusu Liverpool na Mjerumani Klopp, ambaye aliondoka Anfield mwezi Mei.

Video hiyo haijathibitishwa na haijafahamika ni lini ilirekodiwa au uhalisi wake. PGMOL imesema haitatoa maoni yoyote hadi mchakato huo ukamilike.

Liverpool wanafahamu kuhusu video hiyo ambayo imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii lakini klabu hiyo haitazungumzia lolote kutokana na uchunguzi wa PGMOL.