Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alijibu barua za watu marafiki kutoka matabaka mbalimbali nchini Brazil, akiwahimiza kuendelea kuchangia urafiki kati ya China na Brazil.
Katika majibu yake, Xi alisema kuwa anafurahi kuona kwamba urafiki kati ya China na Brazil umerithishwa kutoka kizazi hadi kizazi, na kuongeza kuwa katika miaka 50 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, China na Brazil zimesonga mbele bega kwa bega, zikiwa pamoja kwenye taabu na raha, na wameanzisha urafiki unaovuka milima na bahari.
Amebainisha kuwa China inapenda kushirikiana na Brazil ili kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili katika enzi mpya, na kuufanya uhusiano kati ya China na Brazil kuwa mfano mzuri wa mshikamano, uratibu, maendeleo ya pamoja na kunufaishana kati ya nchi kubwa zinazoendelea, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika amani na maendeleo ya watu.