Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kufanya juhudi za kuwatibu majeruhi waliogongwa na gari siku ya Jumatatu katika mji wa Zhuhai, Mkoa wa Guangdong kusini mwa China.
Katika maagizo yake Xi, ametaka mhusika aadhibiwe vikali kwa mujibu wa sheria. Tukio hilo lilitokea baada ya mtu mmoja kuingiza kwa nguvu gari lake na kugonga watu katika kituo cha michezo huko Zhuhai na kusababisha watu 35 kufariki na wengine 43 kujeruhiwa vibaya.
Xi alizitaka mamlaka husika kupata funzo kutokana na kisa hicho, na kuimarisha kazi za kuzuia na kudhibiti hatari kutoka kwenye chanzo chake.
Pia alisisitiza umuhimu wa kusuluhisha mizozo kwa wakati, kuzuia kutokea kwa matukio makubwa, na kufanya kila juhudi kulinda usalama wa maisha ya watu na utulivu wa kijamii.
Naye waziri mkuu wa China Li Qiang ametoa wito wa kushughulikia ipasavyo tukio hilo, kuchunguza haraka kesi hiyo na kumuadhibu vikali mhusika kwa mujibu wa sheria.