Kampuni za uchimbaji madini za China nchini Zambia zazindua jumuiya ili kukuza michango kwa sekta ya madini
2024-11-13 09:33:32| CRI

Kampuni za China zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini nchini Zambia jana Jumanne zilianzisha jumuiya yao kwa lengo la kukuza michango ya kampuni hizo kwa sekta ya madini nchini humo.

Jumuiya ya Kampuni za Madini za China nchini Zambia (CMEAZ) ilizinduliwa rasmi kwenye sherehe iliyohudhuriwa na balozi wa China nchini Zambia Han Jing, maofisa waandamizi wa Zambia pamoja na wajumbe kutoka kampuni za madini za China.

Kwa mujibu wa balozi Han Jing, sasa nchini Zambia kuna zaidi ya kampuni 20 za madini kutoka China zenye uwekezaji wa zaidi ya dola bilioni 3.5. Amesema, kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni alama wazi ya ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Zambia.