Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo kwenye ziara ya kiserikali mjini Lima nchini Peru na kuhudhuria Mkutano wa 31 wa Viongozi wa jumuiya ya Kiuchumi ya APEC, leo amechapisha makala iliyotiwa saini yenye kichwa "Wacha Meli ya Urafiki kati ya China na Peru Ianze safari" kwenye gazeti la El Peruano.