Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu ya Kenya (KEMRI) imesema imesaini makubaliano ya ushirikiano na kampuni ya dawa ya Tonix ya Marekani, yenye lengo la kusanifu na kutekeleza majaribio ya kikliniki ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa mpox.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo mjini Nairobi, awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo ya mpox ya TNX-801 yatafanyika nchini Kenya, yakilenga kutathmini usalama, uhimilivu na uwezo wa chanjo hiyo wa kuongeza kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa huo.
Mkurugenzi mkuu wa KEMRI, Elijah Songok amesema majaribio hayo yaliyopangwa ya chanjo yanaakisi juhudi za Kenya kuendeleza utafiti wa kisayansi ambao si kama tu utainufaisha Kenya, na bali pia utachangia juhudi za kimataifa za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza yanayoibuka.