Umoja wa Mataifa waanzisha mradi wa kupinga itikadi kali za vurugu katika Afrika Mashariki
2024-11-14 09:25:27| CRI

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) jana Jumatano limeanzisha mradi mmoja wa kujenga amani na kupinga itikadi kali za vurugu kwa ajili ya nchi za Afrika Mashariki.

Mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini Kenya Anthony Ngororano amesema kuwa mradi huo wenye bajeti ya dola za kimarekani milioni 18 unalenga kujenga ustahimilivu wa jamii katika nchi za Kenya, Somalia na Sudan Kusini. Jamii zinazofaidika zitapokea masimulizi na ujumbe wa kupinga matamshi ya chuki, habari potofu na itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu kupitia elimu ya amani katika vyombo vya habari na mazungumzo ya kijamii.

Pia ameongeza kuwa mradi huo wa miaka mitatu unatarajiwa kuimarisha utayari na mwitikio wa jamii kupitia kuboresha taratibu za tahadhari ya mapema ili kukabiliana na itikadi kali za vurugu.