Asilimia kubwa ya wahojiwa duniani watarajia China kuongeza kasi zaidi katika ushirikiano wa Asia na Pasifiki
2024-11-14 10:59:36| cri

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC). Wakati Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Kiuchumi wa APEC ukikaribia, uchunguzi uliofanywa na CGTN unaolenga watumiaji wa mtandao wa kimataifa unaonesha kuwa 86.4% ya waliohojiwa waliipongeza APEC kwa mafanikio yake mazuri katika kukuza ukuaji wa uchumi wa kikanda na kuimarisha ushirikiano wa kikanda, jambo ambalo limeboresha kikamilifu kiwango cha biashara na uwekezaji huria katika kanda ya Asia-Pasifiki, na kufanya eneo la Asia-Pasifiki kuwa jumuiya yenye nguvu zaidi ya uchumi wa kijiografia yenye uwezo mkubwa zaidi wa ukuaji duniani.