Kura ya CGTN: zaidi ya asilimia 80 ya wahojiwa duniani wapongeza mchango wa China katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
2024-11-15 11:01:16| cri

"China itajitahidi kupunguza kiwango cha juu cha utoaji wa hewa chafu kabla ya mwaka wa 2030 na kutimiza uwiano wa utoaji na matumizi ya kaboni kabla ya 2060" "Ifikapo mwaka 2030, uzalishaji wa hewa chafu nchini China kwa kila kitengo cha Pato la Taifa utapungua kwa zaidi ya asilimia 65 ikilinganishwa na 2005"……Katika kukabiliana na changamoto kubwa na vitisho vinavyotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, China inashughulikia suala hilo kikamilifu kupitia hatua madhubuti, na kutoa "suluhu za China" zaidi kwa usimamizi wa hali ya hewa duniani.

Utafiti uliofanywa na Kituo cha Televisheni cha CGTN na Chuo Kikuu cha Renmin cha China, na kupitia Taasisi ya Zama Mpya ya Mawasiliano ya Kimataifa (NEIIC), uliohusisha wahojiwa 7,658 katika nchi 38, umebaini kuwa asilimia 83.5 ya waliohojiwa wanapongeza juhudi na mchango wa China katika usimamizi wa hali ya hewa duniani. Wanaamini kwamba hatua za China katika kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa zimeongeza imani na nguvu katika juhudi za pamoja za kujenga dunia safi na nzuri.