Serikali ya Sudan yasema iko tayari kutatua mapambano na kuhakikisha ufikishwaji wa msaada
2024-11-19 09:06:46| CRI

Serikali ya Sudan Jumatatu ilisema iko tayari kutafuta ufumbuzi wa mapambano nchini humo, na kuhakikisha ufikishwaji wa msaada wa   ubinadamu kwa watu wanaoathiriwa na mapambano.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan ambaye pia ni kamanda mkuu wa Jeshi Abdel Fattah Al-Burhan alipokutana na mjumbe maalumu wa Marekani anayeshughulikia suala la Sudan ambaye yuko ziarani nchini humo Tom Perriello akisisitiza kuwa serikali ya Sudan iko tayari kabisa kwa ufumbuzi wowote wa kukomesha na kutatua mapambano, pia iko radhi kufikishwa kwa msaada wa   ubinadamu, lakini serikali haitaridhia kuwasafirishia waasi silaha badala ya chakula.

Al-Burhan alimwambia Perriello kuwa serikali ya Sudan haikubali kusafirisha silaha kwa Vikosi vya Msaada wa Dharura (RSF) kupitia kituo cha Adre kilichoko kwenye mpaka na Chad.