Shughuli za vyombo vya habari za mawasiliano ya moja kwa moja kati ya vijana wa nchi za Dunia ya Kusini zaanzishwa Rio de Janeiro
2024-11-19 14:49:13| cri

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), kwa kushirikiana na mkutano wa kilele wa vijana wa G20 (Y20) na sekretarieti ya Ikulu ya Brazil, jana Novemba 18 lilianzisha shughuli za Vyombo vya Habari ya Mawasiliano ya Moja kwa Moja kati ya Vijana wa Nchi za Dunia ya Kusini, na kutangaza Azimio la Vyombo vya Habari vya Nchi za Dunia ya Kusini kuhusu Kushirikiana Katika Kuhimiza Ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye  Mustakabali wa Pamoja, ambalo linaungwa mkono na kushirikisha vyombo vya habari 215 kutoka nchi 74.

Akiongea kwenye hafla ya kuanzishwa kwa shughuli hizo , mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema, lengo la kuanzisha shughuli hizo ni kuweka jukwaa la mawasiliano kwa vijana wa nchi za Dunia ya Kusini kushirikiana na kusonga mbele kwa pamoja kwenye nyanja za upashanaji habari, ubunifu wa kisanii, utafiti wa masuala ya kijamii na michezo.