Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala la Sudan ambaye pia ni Kamanda wa Jeshi la Sudan (SAF) Abdel Fattah Al-Burhan Jumanne alisisitiza tena kuwa, Sudan inakataa uingiliaji wowote wa nje unaolenga kulazimisha kutatua mapambano nchini humo.
Akihutubia ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa uchumi unaolenga kukabiliana na changamoto za vita huko Port Sudan Al-Burhan alisema ufumbuzi wa mapambano ni mambo ya ndani, ambao ni kukomesha uasi, kwa kuwa uwepo wake unamaanisha mgogoro utaendelea katika siku za usoni.
Ameongeza kuwa Sudan haitafanya mazungumzo yoyote wala kukubali kusimamisha vita hadi wanamgambo waasi waondoke kabisa katika maeneo waliyoingia. Njia ya serikali ya Sudan ya kukabiliana na mgogoro wa silaha ni pamoja na kusitisha mapambano, kuwahamishia waasi kwenye maeneo mahususi, na kuanzisha mchakato wa kisiasa ili kumaliza muda wa mpito kupitia kuunda serikali ya raia kwa njia ya mazungumzo kati ya wasudan.