Xi asema China na Ufaransa zinabeba majukumu ya pamoja huku kukiwa na mabadiliko mapya katika mazingira ya kimataifa
2024-11-20 10:14:10| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema China na Ufaransa zina wajibu wa nchi kubwa   wa kufanya jumuiya ya kimataifa kuwa na mshikamano ili  kukabiliana na changamoto za kimataifa katika wakati ambao mabadiliko mengi mapya yanajitokeza katika mazingira ya kimataifa.

Xi ameyasema hayo alipokutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika wakati wa kufanyika kwa Mkutano wa Viongozi wa G20 huko Rio de Janeiro, Brazil. Ameeleza  kuwa uhusiano kati ya China na Ufaransa una umuhimu wa kipekee wa kimkakati na ushawishi duniani kwani nchi zote mbili ni zinazojitawala , zilizokomaa na zinazowajibika,  mwezi Mei mwaka huu, yeye na Macron walitoa  matarajio  juu ya miaka 60 ijayo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na  kutoa suati kwa pamoja juu ya changamoto za kimataifa na matatizo makubwa mbalimbali , na  kupata ushawishi duniani. .

Kwa upande wake, Macron amesema Ufaransa inapenda kushirikiana na China kutekeleza kwa makini maoni ya pamoja yaliyofikiwa na  marais wawili wa nchi, kuendelea kuimarisha mawasiliano  kwenye ngazi ya juu, kuimarisha mawasiliano kati ya watu, kuendeleza urafiki wa jadi na  kujenga uhusiano wa aina mpya kati ya nchi na nchi.