Wizara ya afya nchini Kenya yazindua mpango wa kukabili vifo vya watoto wachanga
2024-11-20 23:21:54| cri

Wizara ya Afya nchini Kenya imeimarisha juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini humo baada ya kuzindua mwongozo mpya kuhusu utunzaji wa watoto hao.

Mwongozo huo uliozinduliwa mwanzoni mwa wiki hii katika Chuo cha Mafunzo ya Matibabu (KMTC) Homa Bay, unalenga kuwapa wahudumu wa afya ujuzi wa kuwatunza watoto hasa wanapozaliwa kabla ya wakati.

Waziri wa Afya wa Kenya, Dkt. Deborah Barasa, Mkurugenzi wa Afya Patrick Amoth na Gavana Gladys Wanga, walizindua rasmi vifaa na mwongozo kuhusu jinsi ya kuwatunza watoto wachanga.

Dkt Barasa amesema, kuzaliwa kabla ya wakati ndio kiini cha vifo vya watoto wachanga nchini humo, huku takwimu zikionyesha kiwango cha vifo vya watoto wachanga kuwa 21 kwa kila watoto 100 wanaozaliwa wakiwa hai.