Jeshi la Polisi nchini Tanzania linawashilikia na kuwahoji kwa kina mkazi wa Mikocheni, Diva Gissele Malinzi (36), na Jenifer Jovin Bilikwija (25), mkazi wa Salasala Kinondoni, Dar es Salaam, kwa tuhuma za kukusanya fedha kwa kutumia akaunti zao binafsi kwa ajili ya waathirika wa kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam Novemba 16.
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam SACP Muliro Muliro amesema kitendo hicho ni kinyume cha Sheria na Kanuni zinazoshughulikia majanga.
Amesema jeshi hilo litashirikiana na Mamlaka nyingine za kisheria kuona hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.