Kampuni ya teknolojia ya China Huawei imesaini makubaliano na kampuni ya bima ya Kupa Kenya ili kutoa ufumbuzi wa huduma kwa wateja kwa teknolojia ya akili bandia (AICC).
Ofisa mkuu mtendaji wa Kupa Kenya, John Onyango Otolo, aliviambia vyombo vya habari kuwa ufumbuzi wa teknolojia kutoka Huawei utawezesha kampuni yake kuongeza kwa kiasi kikubwa uzoefu kwa wateja. Pia ushirikiano wao utaboresha ufanisi wa gharama kwa kuwawezesha kuhudumia wateja wengi kwa kutumia wafanyakazi wachache . Aidha amesema teknolojia hiyo itatekelezwa kwa awamu na kurekebishwa ili kusaidia lugha za ndani na kuhudumia wateja wengi zaidi.
Naye mkurugenzi wa uwasilishaji na huduma wa Huawei Kenya, Lin Xiaonan, alisema kuwa ufumbuzi wa AICC unaoandaliwa na Huawei utawezesha Kupa Kenya kupanua shughuli zake za kituo cha simu na hivyo kuhudumia wateja wengi zaidi kwa ufanisi.