Rais Xi Jinping wa China amesema ushuru ulioongezeka wa Umoja wa Ulaya kwa magari ya umeme ya China unafuatiliwa duniani kote, ambapo China siku zote inasisitiza kutatua tofauti kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, huku ikitarajiwa kuwa Ujerumani itaendelea kufanya kazi yake muhimu katika suala hili.
Rais Xi ameyasema hayo kawenye mkutano wake na Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani katika wakati wa kufanyika kwa Mkutano wa Viongozi wa G20 huko Rio de Janeiro, Brazil, akisistiza kuwa China inaiona Ulaya kama nguzo muhimu katika dunia yenye ncha nyingi, na kuongeza kuwa China imejitolea kushirikiana na Ulaya ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja na kukuza maendeleo endelevu na thabiti ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.
Kwa upande wake Chansela Scholz pia alieleza matumaini kuwa EU na China zitatatua suala la magari ya umeme haraka iwezekanavyo kupitia mazungumzo na majadiliano, akisema kuwa Ujerumani inapenda kufanya juhudi katika suala hili.