Kenya yatarajia kuimarisha ushirikiano na China katika utalii na utamaduni
2024-11-21 10:39:35| CRI

Habari za wakati huu msikilizaji na karibu sana kwenye kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CGTN Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi hiki tuna habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, na pia tutakuwa na ripoti inayohusu matumaini ya Kenya ya kuimarisha mawasiliano na China katika sekta za utalii na utamaduni. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CGTN Idhaa ya Kiswahili Nairobi na yatazungumzia muungano wa Taasisi za Confucius za barani Afrika ambao utazileta pamoja taasisi hizo zitakazoshirikiana kukuza lugha ya Kichina katika bara hilo.